Wednesday, 2 March 2016

SHETTA AFUNGUKA KUHUSU GARI LAKE, NA KITENDO CHA KUIGIZWA AKISHIKWA MAKALIO


Baada ya msanii Nay wa Mitego kuachia wimbo wake wa shika Adabu Yako yamesemwa mengi katika mtandao ya kijamii, kutokana na msanii huyo kutumia kipaji chake kuwachana mastaa mbalimbali hapa Bongo akiwemo Shilole, Snura, Wema Sepetu, Ray, Niva, Shetta na wengine wengi.

Katika hao mastaa aliowataja kwa majina kwenye ngoma yake wapo walioibuka na kujibu tuhuma kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia vyombo vya habari au kurasa zao za Instagram, huku wakionesha kuto pendezeshwa na kitendo cha msanii huyo kuwachana na kuwafanya waonekane tofauti mbaele ya jamii inayo wazunguka.

Kwa upande wake mmoja wa wasanii ambao wametajwa katika ngoma hiyo Shetta hitmaker wa Shikorobo, amekuwa na mtazamo tofauti kuhusu nyimbo  na video ingawa katika nyimbo hiyo ametajwa kununuliwa gari na tajiri mmoja ambaye ni mdau wa burudani maarufu kama Chief Kiumbe, na katika video hiyo anaonekana mwanaume aliyeigiza kama Shetta akishikwa makalio jambo ambalo limezua mjadala na mitazamo tofauti.



Shetta amefungukia suala hilo katika mahojiano yake na kipindi cha Planet Bongo cha East Afrika Radio na kueleza kuwa Nay ni rafiki yake wa muda mrefu hivyo hawana tatizo lolote na kilichooneshwa kwenye video ya shika Adabu Yako kwake ni kichekesho, huku akisisitiza kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa gari na anazo nyaraka zote kuthibitisha hilo, huku akieeleza kuwa huenda Nay hakujua kuhusu gari lake ndio maana akaamua kuimba hivyo.

Wednesday, 27 May 2015

MTOTO WA BABA WA TAIFA AONESHA NIA YAKE YA KUGOMBEA URAIS

Kupitia urasa wake wa Facebook Charles Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto wa hayati baba wa taifa Mwalimu JK Nyerere

 ameandika ujumbe mfupi ulioambatana na taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu nia yake ya kutaka kugombea urais kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM



Ndugu zangu watanzania, taifa letu lipo kwenye mchakato wa uchaguzi, mchakato huu ni msingi mkubwa wa maamzi kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu. Tunaamua hatma ya taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Ni kwa sababu hii mimi Charles Makongoro Julius Nyerere nawakaribisha rasmi kijijini kwetu Mwitongo Butiama, Mara.tarehe 1/6/2015 kuwaelezeni nia yangu ya kuomba ridhaa ya wanaccm nafasi ya kupeperusha bendera ya ccm kuliongoza taifa hili kwa nafasi ya urais.

Monday, 3 November 2014

MAKONDA: MSINIGOMBANISHE NA WARIOBA

 MH. PAUL MAKONDA
Aliyekuwa mjumbe wa bunge maalum la katiba Mh.Paul Makonda,amekanusha vikali
kuhusika na vurugu zilizotokea jana katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Nyerere Foundation, ambapo msemaji mkuu alikuwa  jaji Joseph Warioba.

Makonda amesema hafahamu chanzo cha vurugu hizo na hawajui watu walioanzisha vurugu hizo ila amewafananisha na wahuni wasioitakia mema amani  ya nchi
Makonda ameongeza kuwa amefedheheshwa na kitendo cha kupigwa muandishi wa habari wa BBC Anord Kayanda ambaye alijeruhiwa kichwani na mlemavu wa macho Amoni Mpanju.

Vilevile amelaani kitendo cha baadhi ya watu kumgombanisha na Jaji Warioba na amesisitiza kuwa hana ugomvi na jaji  huyo.
MH.Jaji Warioba akiokolewa na aliyekuwa mjumbe wa bunge maalum la katiba Paul Makonda(aliyemshika kiunoni)

Makonda ameendelea kusema kuwa  ana mahusiano mazuri na jaji Warioba na amewasiliana nae kumpa pole kwa kilichotokea na hakupigwa wala kujeruhiwa, na amehoji kuwa inawezekana vipi kumpiga mtu siku moja kabla  na mkaendelea kuwasiliana nae vizuri.

Makonda amewataka watanzania kuiheshimu midahalo inayoandaliwa na taasisi mbali mbali kwani inatija kwa maendeleo ya taifa la Tanzania.

Friday, 19 September 2014

JUKWAA LA WAHARIRI:JESHI LIFUMULIWE.

Absolum Kibanda
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri nchini, ndugu Absolum Kibanda amelitaka jeshi la polisi lifumuliwe na liundwe upya kufuatia kukithiri kwa vitendo vya kionevu dhidi ya waandishi wa habari, 

Ameyasema hayo kufuatiwa kupigwa kwa waandishi wa habari walipokuwa wakikusanya taarifa kuhusiana na kukamatwa na kuhojiwa kwa Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo  ndugu Freeman Mbowe makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar es Salaam  


Askari wakimzonga mwandishi wa Habari

Kibanda amelaani vikali kitendo hicho na kuwataka jeshi la polisi lijue umuhimu wa  vyombo vya habari kwa jamii,

Pia ameongeza kuwa licha ya kulaani hawataishia hapo wataenda mbele zaidi ili kufanikisha wajibu na taaluma ya uandishi wa habari inaheshimiwa,

Pia watamuandikia barua mkuu wa jeshi la polisi Ernest Mangu juu ya kilichotokea na kusikiliza nini kitatokea,

Vilevile amezitaka taasisi nyingine ikiwemo ya haki za binadamu kulaani na kuwachukulia hatua walioonekana dhahiri wa wakifanya vitendo hivyo.


Thursday, 17 July 2014

Polisi Kusini mwa India wameandikisha kesi ya ubakaji ambapo inadaiwa kuwa mtoto wa shule mwenye umri wa miaka 6 alibakwa na wafanyakazi wawili wa shule moja maarufu mjini Bangaloer.
Uhalifu huo unadaiwa kutekelezwa wiki mbili zilizopita.
Mtoto huyo alibakwa na mlinzi pamoja na mwalimu, lakini kwa sababu ya kuwepo walinzi wengi katika shule hiyo, polisi bado wanachukua muda kuchunguza mlinzi aliyehusika.
Polisi wanasema kuwa mtoto huyo alibakwa tarehe mbili Julai , lakini wazazi wake waligundua hilo siku chache zilizopita baada ya mtoto huyo kulalamika kuumwa na tumbo na kupelekwa hospitalini.
Wakati huo mamia ya wazazi wameandamana nje ya shule wakivunja milango na kupiga mayowe kulaani tukio hilo.

Wednesday, 16 April 2014

MAALIM SEIF ATOA KAULI 7 DHIDI YA MUUNGANO.


1. ‘Pamoja na milima na mabonde, muungano huu umedumu miaka 50, nchi nyingine zilishindwa, lazima tufanye tathmini hasa ya muungano wetu, lazima vijana waelimishwe vp muungano uliundwa, tulianzia vipi’

2.‘Ukitaka upate maenedeleo, yatambue mafanikio yako lakini pia usisahau matatizo yako, ni ni moja.. kufanya vizuri, Sidhani katika Tanzania kama kuna watu hawataki muungano, na kama wapo ni wachache, muungano uendelee ndio la msingi’

3. ‘Sio dhambi watu kuwa na fikra tofauti, sio dhambi hata kidogo kwa sababu hatuwezi wote kuwa na fikra aina moja, Wanaotaka serikali moja wasibezwe, mbili wasibezwe, wanaotaka tatu na serikali ya mkataba wasikilizwe pia’

4. ‘Wako wanaoamini kwamba matatizo ya muungano yako kwenye muundo, tuwasikilize wana hoja gani, Mwaka 1963 Malaysia na Tanganyika maendeleo ya sehemu zote hizi yalikua sawa, mwaka 2014 tujiulize, changamoto kwetu ni vipi tutakua na muungano utakaokua ni chachu ya maendeleo ya haraka, mambo ya 74 ni tofauti na 2014′

5. ‘Tuwe makini sana, sote ni wa nchi moja, tujiepushe na kikundi chochote kuona wao wana haki zaidi, Watanzania wote sawa, wajumbe wa bunge maalum waangalie maslahi ya nchi, muungano huu ni wa nchi 2 zilizokua dola huru na kuungana kwa hiari

6. ‘Tupate katiba ambayo itaondoa migogoro, kero iwe ni historia… hili swala lisiwepo tena, tusiende kwenye maamuzi ya harahaharaka tukasema serikali mbili au tatu bila kuangalia athari zake, katiba ya Znz inasema ni miongoni mwa nchi mbili za muungano, ya Muungano inasema Tz ni nchi moja, huo ni mgogoro’

7. ‘Nadhani Warioba walivyopendekezwa waliona hisia za Znz zilivyo, tunataka katiba itakayotambua usawa wa nchi mbili, hakuwezi kuwa na katiba ambayo itamridhisha kila mtu lakini angalau wengi wao waridhike’.