2.‘Ukitaka upate maenedeleo, yatambue mafanikio yako lakini
pia usisahau matatizo yako, ni ni moja.. kufanya vizuri, Sidhani katika
Tanzania kama kuna watu hawataki muungano, na kama wapo ni wachache, muungano
uendelee ndio la msingi’
3. ‘Sio dhambi watu kuwa na fikra tofauti, sio dhambi hata
kidogo kwa sababu hatuwezi wote kuwa na fikra aina moja, Wanaotaka serikali
moja wasibezwe, mbili wasibezwe, wanaotaka tatu na serikali ya mkataba
wasikilizwe pia’
4. ‘Wako wanaoamini kwamba matatizo ya muungano yako kwenye
muundo, tuwasikilize wana hoja gani, Mwaka 1963 Malaysia na Tanganyika
maendeleo ya sehemu zote hizi yalikua sawa, mwaka 2014 tujiulize, changamoto
kwetu ni vipi tutakua na muungano utakaokua ni chachu ya maendeleo ya haraka,
mambo ya 74 ni tofauti na 2014′
5. ‘Tuwe makini sana, sote ni wa nchi moja, tujiepushe na
kikundi chochote kuona wao wana haki zaidi, Watanzania wote sawa, wajumbe wa
bunge maalum waangalie maslahi ya nchi, muungano huu ni wa nchi 2 zilizokua dola
huru na kuungana kwa hiari
6. ‘Tupate katiba ambayo itaondoa migogoro, kero iwe ni
historia… hili swala lisiwepo tena, tusiende kwenye maamuzi ya harahaharaka
tukasema serikali mbili au tatu bila kuangalia athari zake, katiba ya Znz
inasema ni miongoni mwa nchi mbili za muungano, ya Muungano inasema Tz ni nchi
moja, huo ni mgogoro’
7. ‘Nadhani Warioba walivyopendekezwa waliona hisia za Znz
zilivyo, tunataka katiba itakayotambua usawa wa nchi mbili, hakuwezi kuwa na
katiba ambayo itamridhisha kila mtu lakini angalau wengi wao waridhike’.
No comments:
Post a Comment