Friday, 19 September 2014

JUKWAA LA WAHARIRI:JESHI LIFUMULIWE.

Absolum Kibanda
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri nchini, ndugu Absolum Kibanda amelitaka jeshi la polisi lifumuliwe na liundwe upya kufuatia kukithiri kwa vitendo vya kionevu dhidi ya waandishi wa habari, 

Ameyasema hayo kufuatiwa kupigwa kwa waandishi wa habari walipokuwa wakikusanya taarifa kuhusiana na kukamatwa na kuhojiwa kwa Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo  ndugu Freeman Mbowe makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar es Salaam  


Askari wakimzonga mwandishi wa Habari

Kibanda amelaani vikali kitendo hicho na kuwataka jeshi la polisi lijue umuhimu wa  vyombo vya habari kwa jamii,

Pia ameongeza kuwa licha ya kulaani hawataishia hapo wataenda mbele zaidi ili kufanikisha wajibu na taaluma ya uandishi wa habari inaheshimiwa,

Pia watamuandikia barua mkuu wa jeshi la polisi Ernest Mangu juu ya kilichotokea na kusikiliza nini kitatokea,

Vilevile amezitaka taasisi nyingine ikiwemo ya haki za binadamu kulaani na kuwachukulia hatua walioonekana dhahiri wa wakifanya vitendo hivyo.


No comments:

Post a Comment