Monday, 3 November 2014

MAKONDA: MSINIGOMBANISHE NA WARIOBA

 MH. PAUL MAKONDA
Aliyekuwa mjumbe wa bunge maalum la katiba Mh.Paul Makonda,amekanusha vikali
kuhusika na vurugu zilizotokea jana katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Nyerere Foundation, ambapo msemaji mkuu alikuwa  jaji Joseph Warioba.

Makonda amesema hafahamu chanzo cha vurugu hizo na hawajui watu walioanzisha vurugu hizo ila amewafananisha na wahuni wasioitakia mema amani  ya nchi
Makonda ameongeza kuwa amefedheheshwa na kitendo cha kupigwa muandishi wa habari wa BBC Anord Kayanda ambaye alijeruhiwa kichwani na mlemavu wa macho Amoni Mpanju.

Vilevile amelaani kitendo cha baadhi ya watu kumgombanisha na Jaji Warioba na amesisitiza kuwa hana ugomvi na jaji  huyo.
MH.Jaji Warioba akiokolewa na aliyekuwa mjumbe wa bunge maalum la katiba Paul Makonda(aliyemshika kiunoni)

Makonda ameendelea kusema kuwa  ana mahusiano mazuri na jaji Warioba na amewasiliana nae kumpa pole kwa kilichotokea na hakupigwa wala kujeruhiwa, na amehoji kuwa inawezekana vipi kumpiga mtu siku moja kabla  na mkaendelea kuwasiliana nae vizuri.

Makonda amewataka watanzania kuiheshimu midahalo inayoandaliwa na taasisi mbali mbali kwani inatija kwa maendeleo ya taifa la Tanzania.

2 comments: