Wednesday, 9 April 2014

WATU 22 MBARONI KWA MAUAJI YA WANAWAKE 7


Polisi yawashikilia watu 22 kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha mauaji ya wanawake 7.
 Jeshi  la polisi mkoa wa Mara kwa kushilikiana na raia wema limefanikiwa kuwakamata watu 22  kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kuwachinja na kunyonga wanawake saba kutoka baadhi ya vijiji vya mwambao wa ziwa Victoria  katika tarafa ya Njanja wilayani Butiama mkoani Mara.


Kamanda wa polisi mkoa wa Mara kamishina msaidizi mwandamizi Ferdinand Mtui,amewaambia waandishi wa habari kuwa katika matukio hayo ya kikatili na kinyama watu 10 tayari wamefikishwa mahakamini huku wengine kumi na wawili wakingojea taratibu za kisheria ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.

 Hata hivyo kamanda mtui ameomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha watu wote wanahusika katika mtandao huo wa mauaji ya kikatili ya wanawake kwa imani za kishirikina wanakatwa na kufikishwa katika vyombo vya kisheria,huku akisema tayari mbunge wa musoma vijijini ametoa ahadi ya shilingi milioni moja kwa kila mwananchi atakayelisadia jeshi la polisi kukomesha mauaji hayo.
 Siku mbili za zilizopita  mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Mugango wlayani Butiama Bi Anastazia Mang’ombe aliuawa kwa kumnyongwa na watu wasiojukana kwa kutumia kanga yake akiwa shambani,hatua ambayo ilimfanya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Mh Nimrod Mkono,akiwa eneo la tukio kulaani vikali mauaji hayo huku akimtaka waziri mkuu Mh Mizengo Pinda na rais Jakaya Kikwete,kutumia mbinu za kupambana na ujangili wa wanyamapori katika kupambana na mauaji  hayo ya  wanawake jimboni humo.

No comments:

Post a Comment