Wednesday, 2 April 2014

MUUNDO WA MUUNGANO KUJULIKANA IJUMAA

Kupatikana kwa muundo kumeelezwa na Mwenyekiti huyo kwamba kutafanya mjadala juu ya masuala mengine kuwa rahisi. “Kama mnavyojua sura namba moja, sura namba sita na sura namba nane zina masuala yanayofanana.
Lakini kwa vile kanuni zinatutaka tujadili sura mbili mbili tutaanza na sura namba moja na sura namba sita ambazo zinafanana maana zinazungumzia muundo wa Jamhuri na Muungano.
“Kamati zitakapojadili kuhusu muundo wa Serikali ya Jamhuri na Muungano masuala kama mahakama, dola na mengineyo yatakuwa rahisi kuyaingiza katika rasimu kwa kuzingatia mfumo utakaokuwa umekubaliwa na wajumbe wengi wa Bunge la Katiba,” alisema Sitta.


Marekebisho kanuni yasitishwa


Katika hatua nyingine, Bunge Maalumu la Katiba  limesitisha azma yake ya kuwasilisha marekebisho ya kanuni kama ilivyotangazwa Ijumaa, huku Mwenyekiti Sitta akisema hatua hiyo inatokana na Watanzania kuchoka kusikia wimbo wa kanuni ukiimbwa kila siku bungeni.
“Watanzania wamechoka na mjadala wa kanuni kila siku, hivyo nimesitisha ratiba ya uwasilishaji wa marekebisho ya kanuni na badala yake sasa tutaanza kazi ya kujadili rasimu kwenye Kamati. Kama kuna mgongano wowote wa kikanuni utajitokeza huko mbele tutaangalia namna nzuri ya kuutatua,” alisema Sitta.

Waendelea kukosoa Serikali 3


Wajumbe mbalimbali wa Bunge Maalumu la Katiba, akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Nancy Mrikaria wameendelea kukosoa mfumo wa Muungano wa Serikali tatu wakisema unabeba maslahi ya watu wachache.

Akizungumza  mjini Dodoma, Mrikaria amesema wajumbe hao wameaminiwa na wananchi na wanapaswa kuangalia maslahi ya taifa na kuweka kando itikadi za kisiasa.

Aliasa wajumbe kuacha kung’ang’ania serikali tatu akisema serikali mbili bado zinafaa. “Tusiangalie serikali itakayobeba maslahi ya watu wachache, cha muhimu ni kuangalia serikali yenye maslahi ya watu wengi,” alisema.

Mjumbe mwingine wa Bunge Maalumu, William Ngeleja amesema upo umuhimu wajumbe wa bunge hilo kufanya maamuzi ya kuimarisha muungano na kuacha kuwa na maslahi binafsi yenye lengo la kuvunja muungano. Alisema hayo jana mjini hapa huku akisisitiza kuwa muumini wa serikali mbili.

Ngeleja amesema msingi muhimu wa rasimu ni makubaliano hivyo ni muhimu wajumbe wakafanya uamuzi utakaoimarisha muungano licha ya rasimu kutamka serikali tatu.
“Tubishane na tujadiliane kwa hoja, tunaamua hatma ya Watanzania tutimize wajibu wetu kwani wakati wa kujadili rasimu tutaangalia mambo ya kiasiasa na kisheria pia,” alisema Ngeleja.

Amesema bado serikali mbili zinafaa na jambo la muhimu ni kuangalia changamoto zilizopo na kupatiwa ufumbuzi badala ya kufikiria kuwa na serikali tatu. Amesema kwenye kundi la watu 600 kusitegemewe kuwa na mawazo ya aina moja.


Amesihi Watanzania kuwa na amani na utulivu. Alisisitiza kazi ya kutunga katiba ni ya wananchi wote. Amesema ni halali watu walio nje kuendelea kutoa maoni yao na misimamo tofauti kwani baadaye maoni yanachukuliwa na kuchaguliwa yale yanayofaa na yasiyofaa.











No comments:

Post a Comment